Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Demokrasia ya wazi inahitajika zaidi duniani kote:UM

Demokrasia ya wazi inahitajika zaidi duniani kote:UM

Serikali na mabunge kote duniani yanahitaji kutekeleza zaidi demokrasia ya wazi kwa niaba ya watu wao. Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu kuchagiza demokrasia na utulivu wa kimataifa Alfred de Zayas.

Ameyasema hayo katika kuelekea siku ya kimataifa ya demokrasia inayoadhimishwa kila mwaka Septemba15.

Mtaalamu huyo amesema kwamba demokrasia inamaanisha zaidi ya kupiga kila baada ya kipindi fulani na mara kwa mara, watetezi katika miji mikuu wamekuwa wakishawishi sera na sheria badala ya wapiga kura.

De Zayas ametoa wito wa kuwepo majadiliano zaidi kwa upande wa wabunge , akisema kwamba hisia ya kutengwa katika nchi nyingi imekuwa ikisababisha kutojali, utoro na kutokuwa na Imani.