Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka serikali na biashara Mexico kujihuisha na waathirika wa miradi ya maendeleo:

UM waitaka serikali na biashara Mexico kujihuisha na waathirika wa miradi ya maendeleo:

Kikundi cha kikosi kazi cha wataalamu wa Umoja wa mataifa wanaohusika nja biashara na haki za binadamu , kimeitaka serikali ya Mexico na sekta ya biashara nchini humo kujifunza kutokana na makossa ya nyuma na kuhakikisha kuna kuwa na mjadiliano ya kutosha na watu na jamii zilizothirika na miradi ya maendeleo na operesheni za biashara.

Kikikamilisha ziara nchini humo kikosi kazi hicho Pavel Sulyandziga ambaye ni kiongozi wa kikundi amesema, katika taifa lenye tamaduni mchanganyiko kama Mexico , majadiliano yanahitaji kujumuisha makundi yote katika jamii hasa watu wa asili.

Ameongeza kuwa ili kuzuia hatari au athari mbaya kwa watu hususani wasiojiweza , suaqla hili lisichukuliwe kama mzigo bali fursa ya kuimarisha ushindani na maendeleo endelevu.

Kundi limesisitiza kwamba kila muhusika ni lazima ahusishwe tangu hatua za awali kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na misingi ya biashara na haki za binadamu. Ripoti ya mwisho ya kundi hilo, matokeo mengine ya utafiti na mapendekezo vitawasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu mwezi Juni mwaka 2017.