Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao wa ubunifu wa miji wa UNESCO kukutana Östersund, Sweden

Mtandao wa ubunifu wa miji wa UNESCO kukutana Östersund, Sweden

Mkutano wa 10 wa kila mwaka wa mtandao wa ubunifu wa miji wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO (UCCN) utafanyika kuanzia tarehe14 hadi 16 Septemba mjini Östersund Sweeden.

Mkutano huo utawaleta pamoja wawakilishi Zaidi ya 250 wa mtandao huo kutoka miji 116 wakiwemo mameya 20.

Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutanabaisha shughuli za mtandao, kusaidia sera za miji hasa katika masuala ya utamaduni na ubunifu, lakini pia kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama.

Mkutano utatoa fursa ya kubainisha jukumu la mtandao huo kama muwezeshaji wa maendeleo endelevu katika mazingira ya mijini katika kutekeleza ajenda ya UNESCO ya utamaduni na maendeleo lakini pia ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.