Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia yasaidia Sudan kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Teknolojia ya nyuklia yasaidia Sudan kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Wanasayansi nchini Sudan wanashirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) katika kutafuta njia za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ushirikiano huo ni katika kutumia teknolojia ya nyuklia na mbinu za kisasa ili kuimarisha ubora wa udongo katika kuzalisha mimea ya chakula, kuboresha mifumo ya kilimo, na kukabiliana na wadudu, na kadhalika.

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mamilioni ya watu nchini Sudan, zinadhihirika katika jinsi yanavyodhoofisha ubora wa udongo wanapokuza mimea ya chakula, hadi katika kuenea kwa wadudu wanaobeba magonjwa ya mimea.

Aidha, hali ya hewa isiyoweza kutegemewa, mvua nzito na joto kali, vyote kwa pamoja hutia mashakani upatikanaji wa chakula, maji, afya na vitega uchumi.