Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna hofu dhidi ya ongezeko la matumizi ya kandarasi binafsi za ulinzi

Kuna hofu dhidi ya ongezeko la matumizi ya kandarasi binafsi za ulinzi

Nchi nyingi zinazidi kukabidhi operesheni zake za kijeshi kwa majeshi na kampuni binafsi za ulinzi hali ambayo imeanza kuzusha hofu miongoni mwa wataalamu wa kimataifa wa haki za binadamu.

Mijadala mbalimbali kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo Alhamisi inaangalia athari za kile wanachokiita “ubinafsishaji wa vita” Mijadala hiyo imeandaliwa na kikosi kazi kinachofuatilia masuala ya askari mamluki, hasa katika shughuli za askari wanajulikana kama “askari wa bahati”, wakandarasi binafsi wa jeshi na wapiganaji magaidi wa kigeni.

Kikosi kazi hicho kinatoa taarifa kwa baraza la haki za binadamu na baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Profesa Gabor Rona ni mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho.

(SAUTI YA PROFESA RONA)

“Tumeona ongezeko kubwa , katika sekta binafsi ya jeshi , tunashuhudia nyi nyingi ambazo zinashiriki vita ama nchini mwao au nje wanatumia zaidi makandarasi binafsi wa kijeshi, na hilo linazusha hofu mpya katika masuala ya haki za binadamu”