Afrika yajadili upatikanaji wa maji safi na salama
Mkutano wa sita wa maji kwa bara la Afrika unaendelea jijini Dar es salaam nchini Tanzania, ukiwaleta pamoja wadau mbalimbali wa maji wakiwamo watafiti na taasisi za miradi ya maji.
Maji na huduma za kujisafi ambalo ni lengo namba sita la maendeleo endelevu SDGs , inatajwa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa barani Afrika.
Katika mahojiano na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania, Mtaalamu bingwa wa afya jamii kutoka shirika la afya ulimwenguni WHO Tanzania, Idris Sekibo anaeleza manufaa ya mafunzo na uzoefu unaopatikana katika mkutano huo.
(SAUTI IDRIS)