Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujumuisha watoto walioathirika na vita katika jamii ni muhimu sana:Zerrougui

Kujumuisha watoto walioathirika na vita katika jamii ni muhimu sana:Zerrougui

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kuwasaidia na kuwajumuisha watoto walioathirika na vita vya silaha unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya silaha Bi. Leila Zerrougui kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Shirika la kazi duniani ILO, unajikita katika kubadilishana uzoefu na hatua bora za kuwasaidia watoto kisaikolojia na kuwajumuisha katika jamii.

Akisisitiza kuhusu mada inayojadiliwa Bi Zerrougui amesema ni muhimu sana kwa sababu

(SAUTI YA LEILA ZERROUGUI)

“Ni moja ya vitu vya muhimu sana katika kuponya machungu ya watoto, kuwasaidia kupata njia, kuwaruhusu kurejea katika jamii na kwa famialia zao wakiwa na matumaini, wakiwa na kitu ambacho kitawasaidia kusahau kilichowasibu”