Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 32 cha kamati ya uvuvi kimeanza kwenye makao makuu ya FAO

Kikao cha 32 cha kamati ya uvuvi kimeanza kwenye makao makuu ya FAO

Kikao cha 32 cha kamati ya kimataifa ya uvuvi kimeanza leo kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo FAO mjini Roma Italia.

Kamati hiyo ndio jukwaa pekee la kimataifa ambapo wadau wa kimataifa wa uvuvi wanakutana kujadili matatizo, changamoto na masuala ya uvuvi na kutoka na mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia changamoto hizo.

Kikao hicho kimewaleta pamoja wawakilishi wa serikali, mashirika ya kikanda ya uvuvi, asasi za kiraia, wavuvi, jumuiya ya kimataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, la mpango wa chakula duniani WFP na IFAD.

Katika kikao hicho sula kubwa linalojadiliwa ni uvuvi haramu na njia za kukabiliana nao, ambao kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa FAO Graziano da Silva umeongezeka na unatia hasara kubwa, lakini mkataba wa uvuvi ulioanza kutekelezwa karibuni amesema utakabiliana na changamoto hiyo.

(SAUTI YA GRAZIANO DA SILVA)

"Uvuvi haramu unaweza kufikia hadi tani milioni 26 za samaki kwa mwaka , ikiwa ni zaidi ya asilimia 15 ya samaki wote wanaovuliwa duniani. Makataba wa uvuvi unatoa njia ya ubunifu ya kuweza kukabiliana na tatizo hili kwa kuzuia meli kutumia bandari na kushusha mzigo wao haramu”