Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunashughulikia chanzo cha migogoro Afrika Magharibi-Ibn Chambas

Tunashughulikia chanzo cha migogoro Afrika Magharibi-Ibn Chambas

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili amani Afrika Magharibi ambapo mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika ukanda huo UNOWA, Mohamed Ibn Chambas amelihutubia baraza hilo akielezea hatua zilizopigwa katika kufikia amani na changamoto zinazokabili ukanda huo.

Awali Ibn Chambas amefanya mahojiano maalum na redio ya Umoja wa Mataifa akieleza usaidizi wa UNOWA katika kusaidia ukanda wa Afrika Magharibi kutatua migogoro na usaidizi wa kibinadamu.

Amesema uwepo wa kundi la Boko Haram unasalia changamoto kubwa nchini Nigeria, Cameroon,  Niger na ukanda mzima na kusema kile ambacho Umoja wa Mataifa unakisisitiza.

( SAUTI CHAMBAS)

‘Kufanya kazi na  wadau wengine wa ukanda, kimataifa, na kitaifa katika kusaidia jamii zinazoteseka. Pia kutoa usaidizi wa kibinadamukwa kushirikiana na nchi hizi na muhimu kuanisha vyanzo vya migogoro kama vile jamii zilizotengwa, ukosefu wa fursa na ajira kwa vijana.’’