Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU yatoa Euro milioni 6 kusaidia miji kuhimili majanga

EU yatoa Euro milioni 6 kusaidia miji kuhimili majanga

[caption id="attachment_282950" align="alignleft" width="350"]hapanapalemajanga

Ofisi ya Umoja wa mataifa ya kupunguza hatari ya majanga (UNISDR) na shirika la Umoja wa mataifa la makazi (UN-Habitat)wanalenga kupunguza hasara zitokanazo na majanga katika baadhi ya miji iliyo katika hatari duniani kwa msaada wa Euro milioni 6 kutoka Muungano wa Ulaya (EU) katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Bwana. Neven Mimica, kamishina wa Ulaya kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa na maendeleo amesema kuimarisha udhibiti wa hatari ya majanga ni sehemu muhimu saana kwa ajili ya maendeleo endelevu na suala la kipaumbele katika mkataba wa Sendai.

Ameongeza kuwa anafarijika kuona msaada huo wa Muungano wa Ulaya utasaidia mradi wa kuisaidia miji dhaifu kuwa imara na tayari kukabili majanga, kuelimisha uongozi juu ya hatari zijazo, na kushirikisha watu wanaoishi katika miji hiyo kuhusu upunguzaji wa hatari ya majanga.

Baadhi ya miji itakayonufaika na mradi huo ni pamoja na Kathmandu, Nepal,na Port Villa, Vanuatu.