Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wa IOM wakubali kujiunga na familia ya UM

Nchi wanachama wa IOM wakubali kujiunga na familia ya UM

Familia ya Umoja wa Mataifa muda si mrefu inaweza kupanua wigo wake , nah ii ni kwa sababu maandalizi yanaendelea ya kupata mwanachama mpya, ambaye ni shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Hili linafuatia uamuzi wa mataifa 165 wanachama wa IOM, kutaka kushikamana na Umoja wa Mataifa. Ni uamuzi ambao umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa General Ban Ki-moon.

Afisa wa IOM Leonard Doyle anasema hatua hiyo ni ya kihistoria na ni sanjari na ongezeko la hofu ya kimataifa kuhusu suala la uhamiaji.

(SAUTI YA DOYLE)

"Suala la uhamiaji limeandikwa kwenye maamuzi ya mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris mwaka jana, kuna takribani malengo 10 ya maendeleo endelevu yana mada maalumu kuhususani kwa wahamiaji au mada ndogo zinazowahusu na kuna uamuzi wa baraza kuu la Umoja wa mataifa wa kuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu wahamiaji Septemba. Hivyo ni dhahiri kwamba uhamiaji iumekuwa ni sehemu ya ajenda muhimu katika mfumo wa kimataifa”