Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uamuzi wa China kujiunga na IOM

Ban akaribisha uamuzi wa China kujiunga na IOM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha Uchina kujiunga na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Ban amesema anaamini kwamba China itakuwa mchango mkubwa na muhimu kwa IOM.

Uchina kuwa mwanachama wa IOM ni muhimu hasa katika wakati huu ambapo masuala ya wahamiaji na wakimbizi yanahitaji kushughulikiwa na hatua kuchukuliwa haraka kuliko wakati mwingine wowote.

Naye balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa amesema, Ushirika wa china na IOM utaboresha uwezo wa Uchina kushughulikia masuala ya uhamiaji na kupanua wigo wa ushiriki wake kimataifa katika suala hili.