Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgogoro wa Iraq wawaweka watoto milioni 3.6 hatarini:UNICEF

Mgogoro wa Iraq wawaweka watoto milioni 3.6 hatarini:UNICEF

Watoto milioni 3.6 , ikiwa ni mmoja kati ya watoto watano nchini humo wako katika hatari ya kifo, kujeruhiwa, ukatili wakingono, kutekwa na kuingizwa jeshini kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Ripoti kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Ripoti hiyo “gharama kubwa kwa watoto” inatanabaisha kwamba idadi ya watoto walio hatarini kwa ukiukwaji huo mkubwa , imeongezeka kwa watoto milioni 1.3 katika kipindi cha miezi 18.

Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba watoto zaidi ya milioni nne na nusu wanahitaji msaada wa kibinadamu, huku familia nyingi zikikabiliwa na kuzorota kwa hali ya maisha kufuatia operesheni za kijeshi zinazoendelea Fallujah na viunga vya Mosul. Peter Hawkins ni mwakilishi wa UNICEF nchini Iraq.

(SAUTI YA PETER HAWKINS)

“Kwa sasa kuna watoto milioni 4.7 ambao wameathirika moja kwa moja na vita, watoto 1431 wametekwa katika miaka miwli iliyopita, hao ni watoto 50 kwa wiki. Na tuna ripoti za mara kwa mara mwaka huu watoto kusajiliwa na makundi ya kijeshi “