Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutaendelea kusaidia serikali ya DRC- Sidikou

Tutaendelea kusaidia serikali ya DRC- Sidikou

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ikiwa leo ni miaka 56 tangu uhuru wa nchi hiyo, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umeelezea azma yake ya kuendeleza usaidizi wa kuhakikisha kuna amani na usalama. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Katika sherehe zilizofanyika huko Kindu, jimbo la Maniema, MONUSCO imewakilishwa na mkuu wake Maman Sidikou ambaye amesema miaka 56 ya uhuru ni kipindi muhimu cha kutathmini mwelekeo wa nchi na changamoto zilizosalia.

Amesema MONUSCO itaendelea kushirikiana na jeshi la serikali kusaka vikundi vilivyojihami mashariki mwa nchi na kuimarisha mafanikio ya kidemokrasia yaliyokwishapatiakana.

Mkuu wa mawasiliano wa MONUSCO Charles Bambara akizungumza na wanahabari kuhusu uwepo wa Bwana Sidikou kwenye maadhimisho hayo amesema..

(Sauti ya Bambara)

“Ni vyema MONUSCO kusaidia na kushiriki sherehe hizo na mamlaka za serikali. Na ni kweli kumekuwa na dhana ya kuhoji masuala ya ulinzi na usalama kwa sababu kitovu cha majukumu ya MONUSCO ni ulinzi wa raia na ni kutokana na hilo ndio maana tunakuwa sambamba na serikali ya DRC."