Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaidizi kwa nchi zinazoendelea katika mifumo ya afya haukwepeki: Kikwete

Usaidizi kwa nchi zinazoendelea katika mifumo ya afya haukwepeki: Kikwete

Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa kuhusu jitihada za kimataifa wakati wa mizozo ya kiafya Jakaya Kikwete amesema nchi zinazoendelea zinapaswa kusaidiwa kujenga mifumo ya afya.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Tanzania amefafanua kuhusu mapendekezo ya jopo hilo kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na akisisitiza kuhusu msaada wa kimfumo anasema.

(SAUTI KIKWTE)

Kadhalika amesema pendekezo jingine la jopo ni kuimarisha uwezo wa shirika la afya ulimwenguni WHO na hilo lilidhihirika zaidi wakati wa kushughulikia dharura ya homa kali ya Ebola Afrika Magharibi.

(SAUTI KIKWETE)