Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wanaotaka kuondoka Dadaab watafanya hivyo kwa hiari yao- UNHCR

Wakimbizi wanaotaka kuondoka Dadaab watafanya hivyo kwa hiari yao- UNHCR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limesema kuwa harakati zinaendelea nchini Kenya kuwashawishi wakimbizi wa Somalia wapatao 320,000 walioko katika kambi ya Dadaab, kuihama kambi hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi duniani na kurudi makwao.

Mwishoni mwa wiki, UNHCR ilifanya mazungumzo na wawakilishi wa serikali ya Kenya na Somalia, na sasa inasema kuwa lengo la mwaka huu wa 2016 ni kuona Wasomali wapatao 150,000 wanarudi nyumbani kwa hiari yao.

Kwa mujibu wa UNHCR, wote watawezeshwa kurudi kwa heshima na kwa usalama, hasa kwa kuzingatia kuwa kuna operesheni za kijeshi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab, kama Duke Mwancha, Kaimu msemaji wa UNHCR nchini Kenya

Sauti ya Duke Mwancha.