Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchafuzi wa hali ya hewa ni muuaji asiyeonekana na wa kimyakimya Afrika:UNEP

Uchafuzi wa hali ya hewa ni muuaji asiyeonekana na wa kimyakimya Afrika:UNEP

Uchafuzi wa hali ya hewa unasalia kuwa changamoto kubwa barani Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, takribani vifo 600,000 kila mwaka barani humo huusiana na muuaji huyo asiyeonekana, huku asilimia 23 ya vifo duniani sawa na watu milioni 12.6 hutokana na sababu za kimazingira.

Nalo shirika la afya duniani linakadiria kwamba uchafuzi wa hali ya hewa husababisha vifo milioni 7 kila mwaka duniani.

Uchafuzi wa hali ya hewa unasababishwa na kiasi kikubwa cha gesi na chembe zenye maradha kuchanganyika na hewa, na hivyo kusababish maradhi na vifo kwa binadamu, kuathiri viumbe vingine ama wanyama, mazao ya vyakula na mfumo mzima wa maisha.

Miongoni mwa wachafuzi wa kubwa wa hali ya hewa ni gesi ya ukaa, na gesi chafu za viwandani.