Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wazima milioni 29 wanatumia mihadarati:UNODC

Watu wazima milioni 29 wanatumia mihadarati:UNODC

Karibu asilimia Tano ya watu wazima au watu milioni 250 wenye umri kati ya miaka 15 na 64 wametumia japo aina moja ya mihadarati kwa mwaka 2014.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya kimataifa kuhusu mihadarati iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC.

Ingawa idadi inaonekna kuwa kubwa UNODC inasema haijaongezeka sana katika miaka mine iliyopita ikilinganishwa na idadi ya watu duniani. Ripoti hata hivyo inapendekeza kwamba idadi ya watu wanaochukuliwa kuwa wameathirika na dawa za kulevya imeongezeka sana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita.

Sasa kwa mujibu wa ripoti kuna watu milioni 29 katika kundi hilo ikilinganishwa na takwimu za nyuma za watu milioni 27.

Pia ripoti inasema watu wengine milioni 12 wanajidunga sindano za dawa za kulevya na asilimia 14 kati yao wanaishi na Virusi vya Ukimwi, VVU.