Skip to main content

DRC yakumbwa na homa ya manjano: WHO

DRC yakumbwa na homa ya manjano: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetangaza kwamba ugonjwa wa homa ya manjano umeikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC hususani katika majimbo matatu.

Taarifa ya WHO inasema ugonjwa huo unazidi kusambaa hususani ukanda wa mipakani na maeneo yenye watu wengi kama mjini Kinshasa wenye watu zaidi ya milioni 10. Jimbo jingine lililoathirika ni Kisenso.

WHO inatoa usaidizi wa kukabiliana na homa ya manjano DRC.

Dkt. Sylvie Briand, ni Mkurungenzi wa Kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika WHO.

(SAUTI DK BRIAND)

‘‘Ni vigumu sana kupambana na homa ya manjano ndani ya miji mikuu kwa sababu ya msongamano wa watu lakini pia idadi ya mbu ni kubwa zaidi, lakini habari njema ni kwamba kuna chanjo nzuri ya ugonjwa huu ambayo inafanya kazi vizuri na inakinga kwa muda mrefu pengine hata maishani, na ndio maana chanjo ndio njia msingi ya kupambana na homa ya manjano.’’