Skip to main content

Mpango wa ILO na benki ya dunia waimarisha mazingira ya kazi viwandani

Mpango wa ILO na benki ya dunia waimarisha mazingira ya kazi viwandani

Mpango wa pamoja wa shirika la kazi ulimwenguni, ILO na taasisi moja tanzu ya benki ya dunia, IFC umeboresha mazingira ya kazi kwenye viwanda vya nguo, ngozi na viatu katika nchi ambazo zimeanza kutekeleza.

Mkurugenzi wa ILO anayehusika na mazingira bora ya kazi, Dan Rees amesema mpango huo, Better Work unatekelezwa kwenye nchi nane ikiwemo Haiti, na wao wanawekeza kusadia mfumo bora wa menejimenti na wafanyakazi wanachagua wawakilishi wao wenyewe na matokeo ni kwamba..

(Sauti ya Rees)

“Mazingira bora ya kazi ni mazuri kwa biashara. Kuna uthibitisho mkubwa kutoka Better Work Program kuwa viwanda vyenye mazingira bora ya kazi vinapata faida. Viwanda ambavyo wafanyakazi wake wana furaha, ndiko ambako wafanyakazi wanataka kubaki na kufanya kazi kwa tija.”

Mpango huo ulianzishwa mwaka 2006 ili kuboresha mazingira kwenye sekta ya viwanda inayoajiri watu wapatao Milioni 60 ulimwenguni kote wakifanya kazi katika mazingira duni na hatarishi.