Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu DRC uliongezeka mwezi Mei- Ripoti

Ukiukwaji wa haki za binadamu DRC uliongezeka mwezi Mei- Ripoti

Vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC vimeendelea kushamiri mwezi uliopita wa Mei na kufikia 384 ikilinganishwa na matukio 366 mwezi Aprili.

Kwa mujibu wa ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo, visa vingi zaidi viliripotiwa mashariki mwa nchi hiyo ambapo jimbo la Kivu Kaskazini limeshika nambari moja kwa kuwa na visa 143, ikifuatiwa na Ituri.

Visa husika vya ukiukwaji wa haki za binadamu ni pamoja na kukiukwa kwa haki ya uhuru wa watu na usalama, watu kunyimwa uhuru wa kukusanyika kwa amani, uporaji wa mali, mauaji na watu kuchukuliwa hatua bila kufikishwa mbele ya sheria.