Skip to main content

Zaidi ya nusu ya Wayemen hawana chakula cha kutosha:WFP/FAO

Zaidi ya nusu ya Wayemen hawana chakula cha kutosha:WFP/FAO

Hofu inaongezeka kwa watu wa Yemen , umesema Umoja wa mataifa Jumanne kufuatia taarifa kwamba zaidi ya nusu ya watu wa nchi hiyo hawana uhakika wa chakula.

Katika taarifa ya pamoja ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP, na shirika la chakula na kilimo FAO, zaidi ya watu milioni 14 wametajwa kuathirika kutokana na vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na wasi wa Houthi. Bettina Luescher ni afisa wa WFP

(SAUTI YA BETTINA)

"Ni hali mbaya sana, ni moja ya maeneo magumu sana hapa duniani na moja ya mgogoro mkubwa kabisa wa kibinadamu duniani.”

Vikwazo vya kuingiza bidhaa nchini humo kila siku vimefanya hali kuwa mbaya zaidi, kwa mujibu wa WFP ambayo inasambaza msaada kwa watu milioni tatu kwa mwezi.

Shirika hilo limesema kuharibika kwa bandari na kubadilika kwa hali ya usalama kumeongeza madhila kwa watu wa Yemen.