Skip to main content

Balozi mwema Kipchumba ahaha kutokomeza Polio Kenya

Balozi mwema Kipchumba ahaha kutokomeza Polio Kenya

Harakati za kupambana na ugonjwa wa Polio duniani zinashika kasi kila uchao licha ya changamoto zinazokumba watoa huduma ya chanjo hiyo. Mathalani katika baadhi ya maeneo, watoa huduma hukumbwa na vikwazo vya imani za wananchi husika.

Wengine wao huamini kuwa kwa kusali tu, basi ugonjwa huoutatokomea. Nchini Kenya, katika kaunti ya Kitui, kanisa moja lina imani hiyo. Kwa kutambua madhara ya Polio, Seneta Harold Kipchumba kutoka Kenya ambaye ni balozi mwema wa UNICEF  kutokomeza Polio nchini humo  amefunga safari hadi eneo hilo kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo.

Je alikumbana na masahibu gani? Je kuna mafanikio? Grace Kaneiya anafuatana naye katika safari hiyo.