Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Peter Thomson achaguliwa Rais mpya wa Baraza Kuu

Peter Thomson achaguliwa Rais mpya wa Baraza Kuu

Leo Baraza Kuu limekutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuchagua atakayekuwa Rais mpya wa Baraza hilo katika kikao chake cha 71. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Akiongoza mkutano huo, rais wa Baraza Kuu kwa sasa Mogens Lykketoft ameanza kwa kueleza kwamba Rais atakayechukua nafasi yake kwa kipindi cha mwaka mmoja anapaswa kuwa mwenyeji wa nchi ya eneo la Asia – Pacifiki kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa Mataifa.

Na ndipo Bwana Lykketoft akatambulisha wagombea wawili, Balozi Andreas Mavroyiannis wa Cyprus na Peter Thomson wa Fiji.

Na kisha akahimiza wanachama kupiga kura…

Baada ya dakika chache, akatangaza matokeo…

Peter Thomson , mwakilishi wa Fiji, amekusanya wingi wa kura zilizopigwa na ataongoza kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa .