Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR na Rais wa Kenya wajadili hatma ya wakimbizi wa Somalia Dadaab

Mkuu wa UNHCR na Rais wa Kenya wajadili hatma ya wakimbizi wa Somalia Dadaab

Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) Filippo Grandi amekutana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kujadili hatma ya wakimbizi wa Somalia nchini humo.

Ziara ya Grandi imekuja wakati serikali ya Kenya imesema inataka kuifunga kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Dadaab , inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 350,000 wengi wakiwa ni kutoka Somalia.

Kenya imekuwa ikihifadhi wakimbizi wa Somalia kwa zaidi ya miongo miwili na mwaka 2013 Kenya, Somalia na UNHCR walitia saini makubaliano ya kuwasaidia wakimbizi hao wa Kisomali kurejea nyumbani kwa hiyari, jambo ambalo UNHCR inalisistiza

(SAUTI YA GRANDI)

“Nilifurahi saana kusikia Rais akisema kwamba suluhisho lolote na kurejeshwa nyumbani ni suluhisho bora, na lazima liendeshwe katika namna ya kibinadamu, kiutu na kuheshimu sheria na misingi ya kimataifa”