Skip to main content

Ban alaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Ban alaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi yaliyotokea alhamisi hii dhidi ya kambi ya Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) ambapo askari wa Ethiopia kadhaa waliuawa.

Bwana Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Amepongeza askari wa AMISOM na jeshi la Somalia kwa ushujaa wao katika kudhibiti shambulio hilo na kwa kujituma katika kuhakikisha usalama na utulivu Somalia.

Kwa mujibu wa AMISOM, mamia ya wapiganaji wa al-Shabaab wamekamatwa na wengine wengi kuuawa. Halikadhalika, kiasi kikubwa cha silaha kimekamatwa na kuteketezwa.