Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia wahofiwa kufa maji leo mwambao wa Crete:IOM

Mamia wahofiwa kufa maji leo mwambao wa Crete:IOM

Mamia ya watu huenda wamezama leo Ijumaa wakijaribu kusafiri kwa meli kutoka Misri kuelekea kisiwa cha Crete Ugiriki zimesema duru za habari. Taarifa kamilina Priscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRSICLLA)

Operesheni ya uokozi inaendelea ikihusisha meli na helikopta za Ugiriki kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Endapo itathibitika basi vifo hivyo vitakuwa vya kwanza Ugiriki tangu mwezi Aprili. Joel Millman msemaji wa IOM anafafanua zaidi.

(SAUTI YA JOEL MILLIMAN)

“Naelewa kwamba watu 250 wameokolewa, tumeambiwa 700 walikuwa kwenye meli ilipoondoka Alexandria; idadi isiyojulikana wapo kwenye maji sasa na boti na helkopta  za Ugiriki zinashiriki katika uokozi hivi sasa . Crete katika siku tatu zilizopita imekuwa na shugthuli nyingi na leo shughuli hizo zinaweza kuwa zahma”

Takwimu za IOM zinaonyesha kuwa Crete imekuwa ni eneo jipya kivutio kwa wahamiaji na wakimbizi hasa kutoka Afghanistan, Syria na Iraq.