Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la ukimwi bado linaendeshwa na ukiukwaji wa haki za binadamu:UM

Janga la ukimwi bado linaendeshwa na ukiukwaji wa haki za binadamu:UM

Taarifa iliyotolewa na wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa katika kuelekea mkutano wa ngazi ya juu wa kutokomeza ukimwi utakaofanyika hapa New York Juni 8 hadi 10, wameonya kwamba janga la ukimwi bado linaendeshwa na ukiukaji wa haki za binadamu kote duniani, ikiwa ni pamoja na ubaguzi, unyanyasaji, sheria za kutoa adhabu, sera na mazoea.

Wataalamu hao ambao ni wawakilishi maalumu wa haki ya afya Dainius Pῡras; wa dhidi ya ufukara Philip Alston; wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonović; na mwenyekiti wa kundi la Umoja wa Mataifa la kupinga ukatili dhidi ya wanawake Frances Raday, wamezitaka serikali kote ulimwenguni kuondoa sheria za kutoa adhabu, sera na mazoea, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria zinazoharamisha maambukizi ya VVU, mahitaji ya taarifa ,upimaji wa lazima na kwa wale wanaozuia upatikanaji wa huduma za afya, bidhaa na habari.

Kimataifa wanawake na wasichana bado ndio waathirika wa janga hili, na wanaoishi na VVU wanakabiliwa nja ubaguzi, unyanyapaa na ukatili kuliko wanaume.