Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yaonya kuhusu athari za biashara haramu ya maliasili

UNODC yaonya kuhusu athari za biashara haramu ya maliasili

Aina nyingi za mimea na wanyama ziko hatarini kutoweka kutokana na vitendo vya uhalifu na ujangili wa kimataifa, amesema leo Mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa na Uhalifu UNODC, Yury Fedotov. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Bwana Fedotov amesema hayo wakati wa kuelekea siku ya kimataifa ya Mazingira itakayoadhimishwa tarehe 5 mwezi huo wa Juni, akiongeza kwamba aina 7,000 za maliasili zimekamatwa kwenye nchi 120.

Ameeleza kwamba tatizo sasa ni la kimataifa na linahitaji suluhu na mshikamano wa jamii ya kimataifa.

Aidha Bwana Fedotov amesema kwamba hatari siyo tu kutoweka kwa maliasili hizo, lakini pia kuathirika kwa usalama na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.