Skip to main content

UNICEF yawapatia nuru watoto wakimbizi Tanzania

UNICEF yawapatia nuru watoto wakimbizi Tanzania

Nchini Tanzania, idadi ya wakimbizi kutoka Burundi imefika 138,000, wengi wao wakiwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, maelfu miongoni mwao hawakuambatana na mzazi au mlezi yeyote.

UNICEF kwa ushirikiano na mashirika mengine inawasaidia watoto hao kupata familia za kuwalea na kuwapatia matumaini upya.

Ernest Habonimana na wadogo zake Bahati na Issa ni miongoni mwao. Je wanakummbana na madhila gani? Je wangependa kuwa nani wakiwa watu wazima? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.