Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TEHAMA kupatia vijana fursa za kiuchumi: WEF Kigali

TEHAMA kupatia vijana fursa za kiuchumi: WEF Kigali

Uwekezaji katika elimu ya vijana ni msingi wa kuhakikisha maendeleo barani Afrika hadi vjijini, amesema mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu (UNFPA), Babatunde Osotimehin. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Bwana Osotimehin amesema hayo kwenye mjadala wa kimataifa wa kiuchumi unaomalizika leo mjini Kigali, Rwanda, na kuangazia fursa za kiuchumi kwa bara la Afrika.

Akitoa mfano wa Rwanda ambao asilimia 62 ya watu wana umri wa chini ya miaka 24, Bwana Osotimehim amesema mabadiliko makubwa yanahitajika katika sekta ya elimu ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa ambao tayari kwa mujibu wa wataalam wa uchumi unapitia mapinduzi ya nne ya viwanda, misingi yake ikiwa ni simu za mkononi na teknolojia za habari na mawasiliano au TEHAMA.

Na hivyo amesisitiza umuhimu wa TEHAMA katika kuwapatia ajira vijana wote wanaomaliza masomo.

(Sauti ya Bwana Osotimehin)

“Serikali haina uwezo wa kuwaajiri, sekta binafsi haina uwezo wa kuwaajiri. Kitakacholeta mabadiliko ni ujasiriamali, njia mpya za kufanya biashra, kutumia intanet na nyenzo za TEHEMA ili wabuni ajira zao wenyewe na waweze kuuza bidhaa hizo ndani na nje ya Rwanda.”