Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya Haki za Binadamu yaitaka Gambia iwaachie huru waandamanaji

Ofisi ya Haki za Binadamu yaitaka Gambia iwaachie huru waandamanaji

Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, imeeleza kutiwa wasiwasi mkubwa na hali ya makumi ya waandamanaji waliokamatwa wakati wa maandamano ya amani nchini Gambia, mnamo tarehe 14 na 16 Aprili, katika mji mkuu wa Banjul.

Ofisi hiyo imeongeza kuwa imepokea ripoti kwamba baadhi ya waandamanaji ambao bado wanazuiliwa, wameteswa.

Aidha, duru nyingine za habari zinasema kuwa jamaa za watu hao hawajaruhusiwa kuwatembelea, na kwamba baadhi yao wamezuiwa kupata huduma za matibabu.

Rupert Colville ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Geneva..

“Tunatoa wito kwa serikali iwaachie huru wote waliokamatwa na kuzuiliwa kwa kufurahia haki zao za uhuru wa kujieleza, kutoa maoni, na kuchangamana. Tunakariri pia wito wetu kwa mamlaka za Gambia kuzindua uchunguzi huru katika ripoti za kifo cha Solo Sandeng, mwenyekiti wa kitengo cha vijana katika chama cha upinzani cha Muungano wa Demokrasia (UDP) mnamo Aprili 14”