Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa vyombo vya habari duniani maadhimisho nchini Tanzania

Uhuru wa vyombo vya habari duniani maadhimisho nchini Tanzania

Wakati dunia imeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, upatikanaji wa taarifa umesisitizwa kama msingi ili kuhakikisha kwamba mwananchi anapata taarifa sahihi, anaelimishwa, aidha anaburudishwa, mambo hayo yakiwa ni pembe tatu muhimu za vyombo vya habari katika jamii yoyote.

Nchini Tanzania maadhimisho ya siku hii yamefanyika mkoani Mwanza ambako mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amesisitiza umuhimu wa uhuru wa tasnia hiyo katika kuwapatia wananchi habari ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Bwana Rodriguez  katika ujumbe wake amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na wadau mbali mbali.

Ni katika muktadha huo alitumia maadhimisho hayo kufanya ziara yeye na ujumbe wake kwenye chuo kikuu cha mtakatifu Agostino nchini Tanzania, SAUT. Je nini kilijiri? basi tuungane na Martin Nyoni kutoka radio washirika Radio SAUT  kupata undani wa ziara….