Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji watoto wanaosafiri peke yao wahitaji ulinzi- UNICEF

Wahamiaji watoto wanaosafiri peke yao wahitaji ulinzi- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka hatua za dharura kulinda wakimbizi na wahamiaji watoto huko Ulaya ambao wanasafiri peke yao.

UNICEF imesema watoto hao wako hatarini kukumbwa na manyanyaso, usafirishaji haramu na hata kutumikishwa na idadi yao imevunja rekodi mwaka jana na kufikia zaidi ya Elfu 95.

Shirika la polisi la kimataifa, INTERPOL linasema kati ya watoto hao Tisa, mmoja wao hupotea lakini takwimu inatarajiwa kuwa kubwa.

Sarah Crowe ni msemaji wa UNICEF , Geneva, Uswisi.

(Sauti ya Sarah)

“Mara nyingi mchakato huchukua miezi 11, nasi tunapendekeza upunguzwe hadi miezi mitatu ambapo mtoto atambuliwe, asajiliwe na iwapo ana familia na anasikilizwa kwa maslahi yake ili kubaini iwapo kuna jamaa na iwapo wapo basi aunganishwe nao.”

Idadi kubwa ya watoto wanaosaka hifadhi ni wavulana kutoka Afghanistan ambako wale wa Syria wanashika nafasi ya pili.