Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatari ya maambukizi ya homa ya manjano ni kubwa kwa wasiochanjwa:WHO

Hatari ya maambukizi ya homa ya manjano ni kubwa kwa wasiochanjwa:WHO

Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti kuhusu hali ya homa ya manjano hasa baada ya mlipuko wa homa hiyo nchini Angola mwishoni mwa mwaka jana. Angola imeripoti visa zaidi ya 2,000 vinavyoshukiwa na vifo 277.

Kwa mujibu wa WHO watu wasiopata chanjo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa wakisafiri kwende kwenye nchi zilizoripotiwa kuwa na homa hiyo.

Tangu mwanzo wa mwaka huu WHO imepata taarifa ya visa vya homa hiyo kutoka mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Kenya, China na Uganda. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO

(SAUTI YA TARIK)