Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto ni nyingi Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi:Rugunda

Changamoto ni nyingi Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi:Rugunda

Licha ya juhudi zinazoendelea, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa katika ufadhili wa vipaumbele vya mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha taasisi na nguvu kazi na kutathimini teknolojia ambayo ni muhimu kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi .

Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda alipohutubia kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa Paris kwa niaba ya mataifa ya Afrika.

Bwana Rugunda amezitaka nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi za afrika kushughulikia changamoto hizo kwa minajili ya mkataba wa Paris na ajenda ya kuchua hatua ya Addis Ababa.

Ameongeza kuwa serikali ya Uganda imechukua hatua kadhaa kuhakikisha utekelezaji wa mkataba huo ikiwemo kuhusuicha masuala ya tabianchi kwenye ajenda ya taifa ya “mtazamo wa Uganda wa 2040’. Na akaiasa jumuiya ya kimataifa akisema

(SAUTI YA RUGUNDA)

“Mtazamo wowote ule usio kamilifu au wa kuchagua hautotupa ama kutuhakikishia dunia salama kwa sasa wala vizazi vijavyo. Hautosaidia madhila ya jamii zinazoishi katika mazingira magumu katika nchi masikini , yanayopigania kuokolewa kutokana na kutoweka”