Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upatikanaji wa huduma ya maji mjini Nairobi-Kenya

Upatikanaji wa huduma ya maji mjini Nairobi-Kenya

Uhaba wa maji unaathiri zaidi ya asilimia 40 ya watu kote ulimwenguni, hii ikiwa ni idadi kubwa inayotarajiwa kuongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayochea ukame na kukauka kwa vyanzo vya maji. Licha ya kwamba tangu mwaka 1990  watu bilioni 2.1 wanapata maji na huduma za kujisafi, bado huduma hafifu ya maji safi inasalia changamoto ambayo inaathiri kila bara.

Juhudi za upatikanaji wa maji salama na kwa bei nafuu kufikia mwaka 2030 zinahitaji uwekezaji katika miundombinu ili kuweza kutoa huduma ya kujisafi. Upatikanaji wa maji safi na huduma ya kujisafi ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu ambayo yataweza kufikiwa iwapo kuna juhudi za pamoja.

Moja ya hatua dhahiri ambazo nchi zimechukua ni utiaji saini wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi tarehe 22 mwezi huu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako historia imeandikwa kwa nchi nyingi kutia saini mkataba ndani ya siku moja, nchi 171. Saini zimewekwa na tayari hatua zimeshaanza kuchukiliwa huko ambako mabadiliko ya tabianchi yanachochea uhaba wa maji ikiwemo nchini Kenya. Je ni mikakati ipi ambayo Kenya imejiwekea? Basi tuelekee nchini humo ambako Geoffrey Onditi kutoka radio washirika KBC anatupeleka mtaa wa Kayole ulioko mji mkuu Nairobi.