Mkuu wa OCHA asikitihswa na tetemeko la ardhi Ecuador

17 Aprili 2016

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya kibinadamu OCHA  Stephen O'Brien ameeleza kusikitishwa sana na tetemeko la ardhi lililotokea nchini Ecuador siku ya jumamosi na kusababisha vifo zaidi ya 230 na majeraha wapatao 1,500.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, bwana O'Brien amewapa pole watu zaidi ya milioni moja walioathirika na janga hili, akipongeza jitihada za timu za kitaifa za dharura zinazohaha sasa kuoka maisha ya manusura.

Bwana O'Brien ameeleza kuwa ameanza kuandaa timu ya kutathmini mahitaji na kuratibu misaada inayoongozwa na OCHA huku Shirika la Afya duniani WHO likiwa limetuma timu ya dharura pia.

Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA, tetemeko hilo la ardhi ni kubwa zaidi katika historia ya Ecuador, likiwa limefikia kiwango cha 7.8 kwenye ngazi ya Richter, huku hospitali kadhaa, barabara na nyumba zikiwa zimeteketezwa. 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter