Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waomba hifadhi wa Msumbiji wahamishiwa kambi ya Luwani, Malawi:UNHCR

Waomba hifadhi wa Msumbiji wahamishiwa kambi ya Luwani, Malawi:UNHCR

Huko Kusini mwa Malawi , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanza operesheni kubwa ya kuwahmisha waomba hifadhi wa Msumbiji takribani 10,000.

UNHCR inasema operesheni hiyo iliyoanza asubuhi ya leo ina lengo la kuboresha hali ya maisha ya waomba hifadhi hao.

Kundi la kwanza la waomba hifadhi 81 wameondoka wiolaya ya Nsanje kwa uwa usafiri wa mabasi kuelekea Luwami kusini Mashariki mwa nchji hiyo.

Wakiwasili watawekwa kwenye kambi ya muda kwa siku mbili hadi watakapopewa viwanja, chakula, vifaa vya malazi na vifaa vingine vya nyumbani. William Spindiler ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA SPINDLER)

"Tunawahamisha ni watu walio mpakani, kwani bado watakuwa hatarini, kwa hiyo tunawahamishia ndani zaidi ya Malawi, na hatuna uhakika kama kuna wengine wanaowasili. Watu hawa walikimbia kwa sababu ya mapigano baina ya wafuasi wa RENAMO na  serikali ya FRELIMO."