Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Google na FAO zashirikiana kwa ajili ya misitu

Google na FAO zashirikiana kwa ajili ya misitu

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Kampuni ya Google, zimeamua kuongeza ushirikiano wao ili kuimarisha jinsi ya kutathmini matumizi ya rasimali duniani kote, kupitia satelite na mfumo wa google Earth. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Taarifa hiyo imetolewa wakati ambapo warsha inafanyika wiki hii mjini Roma Italia kwenye makao makuu ya FAO kuwafundisha wataalam wa misitu jinsi ya kutumia google Earth.

FAO imesema kupitia mfumo huo wataalam wanaweza kufuatilia uwepo wa misitu na uwezo wa nchi wa kudhibiti uzalishaji wa kaboni dayoksidi na hivyo kutimiza tathmini hizo kwa saa chache, kawaida zikichuka zaidi ya mwezi.

Halikadhalika, mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema tayari ushirikiano huo umeibua fursa zingine kubwa za ubunifu katika kuimarisha ukusanyaji data kwa ajili ya kufuatilia madhara ya mabadiliko ya tabianchi na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.