Skip to main content

Syria: awamu nyingine ya mazungumzo yaanza Geneva

Syria: awamu nyingine ya mazungumzo yaanza Geneva

Mazungumzo ya amani ya Syria yanaanza tena leo mjini Geneva Uswisi, yakihamasishwa na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Awamu hii nyingine ya mazungumzo inatarajiwa kuendelea kwa muda wa siku kumi, ambapo wawakilishi wa pande kinzani hawatajadiliana ana kwa ana ila kupitia Bwana De Mistura.

Kwa mujibu wa Redio ya Umoja wa Mataifa nchini Uswisi, mazungumzo yataanza leo na ujumbe wa upinzani, huku ujumbe wa upande wa serikali ukitarajiwa kuwasili Geneva baada ya uchaguzi wa wabunge unaofanyika leo nchini Syria.

Bwana de Mistura ambaye ametembelea Syria na Iran wili iliyopita anategemea kuzungumzia suala la msingi la mchakato wa mpito wa kisiasa.