Wahamiaji wengi wawasili Niger wakitokea Libya

Wahamiaji wengi wawasili Niger wakitokea Libya

Ripoti zinasema kuwa kiasi cha watu 4,900 wamewasili nchini Niger wakitokea Libya na maelfu wengine wanasadikika wapo njiani kuelekea kaskazini wa Nigeria katika mji wa Dirkou ama watakuwa wamekwama katika mji wa Sabha ulioko kusini mwa Libya.

Maafisa wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM walioko mjini Dirkou wamedokeza kuwa kuna misafara mikubwa ya watu wanaoendelea kuwasili kwenye eneo hilo na hali hiyo inategemewa kuongezeka zaidi katika chache zijazo.

Taarifa zaidi zinasema kwamba maelfu ya wahamiaji wengine wameendelea kukwama katika mji wa Sabha kutokana na kukosa msaada wa dharula. Katika hatua nyingine shirika hili la Umoja wa Mataifa IOM linaendelea na shughuli yake ya uokoaji wa kwa  wahamiaji wengine waliokwama mpakani mwa nchi za Tunisia na Misri.