Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya kuongezeka machafuko ya magenge

UNHCR yaonya kuongezeka machafuko ya magenge

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesikitishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wanokimbia machafuko ya megenge Amerika ya Kati, ambayo yanadaiwa kuwa makubwa ikilinganishwa na miaka 30 iliyopita.

UNHCR imesema inahofia idadi ya wanawake na watoto wasiosindikizwa ambao huishia kujumuishwa na makundi hayo, kukumbwa na mashambulizi ya kingono au mauaji.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa kuna kiwango cha juu cha machafuko katika nchi hizo kinachoongeza kiwango cha kusaka hifadhi.

Amesema kwamba kuna haja ya kuwa na mkakati na mbinu jumuishi katika kutatua changamoto hiyo. Nchi zinazofikiwa na wasaka hifadhi kufuatia machafuko ya magenge ni Mexico, Costa Rica na Marekani.