Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kobler alaani mauaji ya raia Libya

Kobler alaani mauaji ya raia Libya

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler, amelaani mauaji yaliyoripotiwa kufanyika Mashariki mwa Libya kwenye maeneo ya al-Tewibya na al-Zawiya.

Bwana Kobler amesema kwamba mauaji hayo ya raia ni ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu.

Taarifa iliyotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL imeeleza kwamba vikundi vilivyojihami vimeripoti kuteka nyara wanaume kadhaa, kuwaua, pamoja na kuua na kujeruhi raia wengine wakiwemo watoto.

Bwana Kobler ametuma salamu zake za rambi rambi kwa familia za wahanga akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.