Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazindua filamu kuhusu hali halisi ya watoto wakimbizi

UNICEF yazindua filamu kuhusu hali halisi ya watoto wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF), linazindua leo filamu zinazolenga kutoa picha halisi ya watoto wakimbizi na wahamiaji, kwa minajili ya kuwashawishi watu wawe na mtazamo mzuri kuhusu makumi ya mamilioni ya watoto na vijana walio kwenye safari za ukimbizi au uhamiaji.Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Joseph)

Filamu hizo tatu ziitwazo “Unfairy Tales”ni hadithi halisi za watoto wanaokimbia mizozo, zikieleza vitisho vilivyowapelekea kukimbia.

Filamu hizo ni sehemu ya mkakati wa #actofhumanity, ambao unasisitiza kuwa watoto ni watoto, na kwamba kila mtoto ana haki zake na anastahili kupewa fursa nzuri, bila kujali anakotoka.

Ingawa ni hadithi halisi, filamu hizo zimeundwa kwa njia ya hadithi za watoto za kubuni, na zimewekwa pia kwenye kitabu cha elektroniki kiitwacho Unfairy Tales.