Ban alaani shambulizi la bomu Lahore, Pakistan

28 Machi 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulio la bomu la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye bustani ya Gulshan-e-Iqbal katika mji wa Lahore, nchini Pakistan, ambalo liliwaua watu wapatao 60 na kujeruhi zaidi ya 100 wengine, wakiwemo wanawake wengi na watoto.

Taarida ya msemaji wake imesema Katibu Mkuu ametoa wito waliotekeleza shambulio hilo wafikishwe hima mbele ya sheria, kulingana na kanunui za haki za binadamu.

Ban ametoa wito kwa serikali ya Pakistan kufanya kila iwezalo kuchukua hatua za ulinzi na kuhakikisha usalama wa kila mtu, zikiwemo jamii za walio wachache kidini nchini humo.

Katibu mkuu ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga, na kueleza mshikamano wake na watu na serikali ya Pakistan.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter