Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adama Dieng aeleza kuridhishwa na hukumu ya Karadzic

Adama Dieng aeleza kuridhishwa na hukumu ya Karadzic

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, ameeleza kuridhishwa na hukumu iliyotolewa leo na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani ICTY ya dhidi ya Rais wa zamani wa Jamhuri ya Serbia na kamanda wa jeshi la Serbia kutoka Aprili 1992 hadi Julai 1996.

Karadzic amekutwa na hatia ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa vita, na amehukumiwa kwenda jela miaka 40.

Bwana Dieng amesema, leo ni sku ya kihistoria, na kwamba hukumu dhidi ya Karadzic inatuma ujumbe dhahiri kuwa ukwepaji sheria hautashamiri, na kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Dieng amesema hukumu hiyo siyo tu kuhusu yaliyopita, bali pia ni kuhusu siku zijazo, akiongeza kuwa uwajibikaji ni sehemu muhimu ya kuzuia na pia hatua muhimu katika maridhiano ya kitaifa baada ya mzozo.