Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kukata tamaa Iraq yaweza kuwa tiketi ya maelfu kuondoka :Ging

Hali ya kukata tamaa Iraq yaweza kuwa tiketi ya maelfu kuondoka :Ging

Kuna uwezekano wa msafara mkubwa wa Wairaq kukimbia endapo ufadhili hautopatikana kuwasaidia maelfu walio katika hali mbaya ya kibinadamu,  ameonya leo afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa.

John Ging, ambaye ni mratibu wa operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa kote duniani amesema , Wairaq zaidi ya milioni 10 wanahitaji msaada wa haraka katika taifa hilo lililoghubikwa na vita. Hadi sasa ombi la Umoja wa Mataifa la dola milioni 861 kwa ajili ya Iraq limefadhiliwa asilimia 15 tu.

Akiwa ndio amerejea tu kutoka Iraq Ging amesema nchi hiyo inachohitaji ni kusaidiwa na sio kugawiwa. Tathmini hiyo imekuja baada ya kutembelea wakimbizi wa ndani ambao wako milioni 2.4. akisema watu hao wamemaliza kila kitu na wakalazimika kwenda kwenye makambi ya muda ambayo kwa sasa yapo 3700 nchini humo.

Amesema wairaq hivi sasa ndio wanashika nambari tatu kwa kundi kubwa lwa wakimbizi wanaoingia Ulaya.