Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid alaani mfululizo wa mashambulizi ya anga Yemen

Zeid alaani mfululizo wa mashambulizi ya anga Yemen

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amelaani mfululizo wa mashambulio ya anga nchini Yemen ambayo amesema yanaendelea kusababisha madhila kwa wananchi wa taifa hilo lenye mgogoro.

Akiongea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Zeid amelaani pia hatua ya serikali ya mpito  kushindwa kuchukua kuzuia kujirudia kwa mashambulizi na kuitaka kufanya uchunguzi huru, kuchapisha hadharani matokeo ili kuzuia matukio ya mashambulizi ya awali.

Amesema mauaji yaliyosababishwa na mashambulizi katika soko la Al Khamees Kaskazini Mashariki mwa Yemen Jumanne yalikuwa moja ya matukio katili tangu kuanza kwa mgogoro  mwaka mmoja uliopita

Katika shambulio hilozaidi ya watu 100 waliuwawa wakiwamo watoto 24.