Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili hali Burundi, Ban asema ni wakati wa utekelezaji

Baraza la usalama lajadili hali Burundi, Ban asema ni wakati wa utekelezaji

Baraza la usalama leo limekutana kujadili hali nchini Burundi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelihutubia baraza hilo akisema baada ya ziara yake nchini Burundi kinachotarajiwa sasa ni utekelezaji wa yale waliyokubaliana na Rais Piere Nkurunziza.

Ban amesema uachiwaji huru wa wafungwa wa kisiasa na ukomeshwaji wa vikwazo kwa asasi za kiraia na mashirika ya habari ni moja ya hatua tarajiwa.

Naye Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa  Zeid Ra’ad Al Hussein, akihutubia baraza la usalama amesema licha ya ishara chanya za hivi karibuni kufuatia ziara ya ujumbe wa baraza la usalama, Katibu Mkuu, bado kuna mengi ya kufanwa ilikufikia amani ya kweli Burundi.

Amesema pamoja na viongozi hao kadhalika wakuu watano wa nchi za Afrika, na wasaidizi wa wawili wa Katibu Mkuu wa UM na wataalamu huru wa baraza la haki za binadamu walifanay ziara nchini humo na akaongeza kwamba  ufutailiaji zaidi unahitajika kwa hatua madhubuti za kujihusisha kikamilifu katika upatanisho.

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York Balozi Tuvako Manongi amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki itandeleza juhudi za kusaidia amani na usalama nchini Burundi kwa kuwa mgogoro huo usiposhughulikiwa utakuza zaidi madhara ya kibinadamu.

Akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyoitoa mwaka 2000 katika juhudi za uptanishi wa mgogoro wa Burundi ambapo alitaka suluhu ipatikane kwa majadiliano jumuishi, Balozi Manongi amepongeza uteuzi wa kiongozi huyo kuwa mwezeshaji wa majadiliano ya amani nchini Burundi.

Katika mahojiano na idhaa hii baada ya kulihutuibia baraza hilo balozi Manongi amesema kiel ambacho jumuiya kimataifa inapaswa kufanya.

( SAUTI BALOZI)